Mshukiwa Sugu Wa “Ugaidi “Anaswa Mombasa.

Mshukiwa Sugu Wa “Ugaidi “Anaswa Mombasa.

by -
0 542

Polisi wa kukabiliana na ugaidi wakisaidiwa na wale wa kupambana na ghasia wamemkamata mshukiwa wa ugaidi anayetajwa kuwa sugu eneo la Bondeni hapa Mombasa.

Mshukiwa, sheikh Khalid Mohammed ambaye amekuwa akifuatiliwa na polisi kwa muda mrefu, anadaiwa kuwasajili vijana wanaojiunga na kundi la alshabaab nchini Somalia.

Polisi pia walipata guruneti inayotengenezwa nchini urusi na kifaa kinachotumika kulipua.

Mshukiwa alikuwa akihubiri katika msikiti wa papa mji wa Old Town hapa Mombasa.

Comments

comments