Mshukiwa Sugu Wa Ugaidi Akamatwa Mombasa

Mshukiwa Sugu Wa Ugaidi Akamatwa Mombasa

by -
0 561

Polisi wa kukabiliana na ugaidi wakisaidiwa na wale wa kupambana na ghasia wamemkamata mshukiwa wa ugaidi eneo la Bondeni hapa Mombasa.

Jina la mshukiwa limetolewa kama Khalid Mohammed na polisi wanamtaja kuwa mshukiwa sugu wa ugaidi.

Amekuwa akifuatiliwa na polisi kwa muda mrefu na anadaiwa kuwasajili vijana wanaojiunga na kundi la al-shabaab.

Polisi pia wamepata Guruneti inayotengenezwa nchini Urusi na kifaa kinachotumika kulipua.

Polisi pia wamepata gari katika msitu wa Boni huko Lamu, linalomilikiwa na mshukiwa na linaaminika kutumika kusafirisha mabomu na PIA chakula.

Comments

comments