“Juju”Yatumika Kupeleka Wanawake Wakenya Kufanya Kazi Uarabuni.

“Juju”Yatumika Kupeleka Wanawake Wakenya Kufanya Kazi Uarabuni.

by -
0 605

Madai yameibuka kuhusu mawakala wanaotumia ushirikina ili kusajili wanawake kutoka hapa pwani, kwenda kufanyakazi katika mataifa ya uarabuni.

Watetezi wa haki za kibinadamu, walisema mbinu hiyo ambayo pia inatumika Afrika Magharibi hasa Nigeria, imechangia pakubwa ulanguzi wa binadamu.

Katika mahojiano ya kipekee na Baraka FM, msichana mmoja ambaye jina lake tumelibana, alieleza masaibu aliyopitia katika nchi za Qatar na Libya.

Utafiti wa shirika la kimataila la Uhamiaji –IOM umetaja Kenya kushuhudia visa vingi vya ulanguzi wa binadamu miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, ni takriban elfu 17 kila mwaka.

Visa vya wakenya hasa wanawake kuteswa au hata kuuawa wakifanyakazi nchi za Uarabuni hasa Saudia vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara humu nchini,idadi kubwa ya wahanga wakitoka hapa pwani.

Comments

comments