Polisi Watumia Ndege Kusaka Wahalifu Kilifi.

Polisi Watumia Ndege Kusaka Wahalifu Kilifi.

by -
0 406

Vikosi vya usalama kaunti ya Kilifi vinaendeleza oparesheni ya angani kusaka wahalifu wanaokisiwa kujificha katika misitu mikubwa kaunti hiyo.

Kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Douglas Kanja, alisema operesheni hiyo inafuatia taarifa kutoka kwa wananchi kuwa watu wanaoshuku mienendo yao, huonekana katika misitu hiyo wakifanya mazoezi ya kivita.

Kanja alisema wanalenga zaidi misitu ya Arabuko, Mwarakaya, Kaya Jibana na Kayafungo ambayo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikidaiwa kutumiwa na wafuasi wa kundi la Mombasa Republican council-MRC kwa mafunzo ya kivita.

Kundi la MRC lilipigwa marufuku na serikali likitajwa kuwa kundi haramu.

Comments

comments