Mwanafunzi Aliyetekwa Nyara Taita Taveta Atibiwa Kijabe.

Mwanafunzi Aliyetekwa Nyara Taita Taveta Atibiwa Kijabe.

by -
0 341

Mwanafunzi wa kike aliyetekwa nyara mapema mwezi huu katika kaunti ya Taita Taveta, anauguza majeraha katika hospitali ya Kijabe.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 ni mwanafunzi wa kidato cha pili, na alitekwa nyara na watu walioshukiwa kuwa washirika wa mtandao wa kigaidi.

Alipatikana juma lililopota katika mtaa wa Estleigh mjini Nairobi akiwa na majeraha, baada ya kuanguka kutoka jumba la orofa alilofungiwa na waliomteka nyara.

Mwanamume mmoja aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo anafikishwa mahakamani Nairobi Jumatatu, kujibu mashtaka ya ubakaji, utekaji-nyara, na pia madai ya ugaidi.

Polisi iliwasiliana na familia ya msichana huyo ambaye tayari amefanyiwa upasuaji wa kimatibabu, katika hospitali hiyo ya Kijabe.

Comments

comments