Mbunge Atishia Kuishtaki Mamlaka Ya Viwanja Vya Ndege Kuhusu Fidia.

Mbunge Atishia Kuishtaki Mamlaka Ya Viwanja Vya Ndege Kuhusu Fidia.

by -
0 353

Viongozi katika kaunti ya Lamu sasa wanataka Mamlaka ya kusimamia Viwanja vya Ndege nchini KAA, kuwafidia wale ambao ardhi zao zilitwaliwa kupanua uwanja wa ndege wa Manda.

Mbunge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa, alipendekeza KAA kuwafidia waathiriwa hao kwa kima cha shilingi milioni 1.5 kwa ekari moja.

Hata hivyo Ndegwa aliwataka wakazi wa eneo hilo kushirikiana ili kufanikisha upanuzi huo.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Manda, mbunge huyo alidokeza kwamba ameskitishwa na hali ya wenye ardhi hizo ambapo hadi leo hawajafidiwa.

Alitishia kuelekea kortini kuwasilisha kesi ya kulazimisha KAA kuwafidia wakazi hao walitoa ardhi yao kwa upanuzi wa ardhi.

Comments

comments