Baa La Njaa Laripotiwa Kaunti Ya Taita Taveta.

Baa La Njaa Laripotiwa Kaunti Ya Taita Taveta.

by -
0 381

Zaidi ya watu elfu 60 kati ya laki tatu katika kaunti ya Taita Taveta, wanasemekana kuathirika na baa la njaa.

Akizungumza kwenye mkutano na maafisa wanaohusika na usalama wa chakula mjini Wundanyi, Gavana wa kaunti hiyo, John Mruttu, alisema maeneo yaliyoathirika zaidi na njaa ni yale yaliyoko nyanda za chini.

Mruttu alisema mtu mmoja kati ya watu watano analala njaa na hali hiyo imeathiri hata mifugo kufuatia kiangazi kikubwa kinachokumba sehemu hiyo.

Hata hivyogavana huyo, alilaumu uharibifu wa misitu kuwa umechangia kupotea kwa chemichemi za maji.

Kufutia hali hii serikali hiyo ikishirikiana na shirika la Africalead imeanzisha mafunzo ya wiki mmoja kuelimisha wananchi kuhusu usalama wa chakula.

Katika mafunzo hayo wananchi pia wanafunzwa jinsi ya kujihusisha na ukulima wa kisasa ili kupata chakula cha kutosha.

Comments

comments