Washukiwa 35 Wa Uhalifu Wakamatwa Mombasa.

Washukiwa 35 Wa Uhalifu Wakamatwa Mombasa.

by -
0 387

Polisi wakisaidiwa na askari wa kaunti ya Mombasa wamewakamata vijana 35 eneo la Magongo na Potreize wilayani Changamwe kufuatia oparesheni ilioendeshwa alhamisi usiku.

Wawili kati ya washukiwa hao waliokamatwa ni raia wa Somalia ambao walipatikana na Sacheti 20 ya dawa za kulevya aina ya heroine.

Washukiwa wanahusishwa na visa kadhaa vya uhalifu maeneo kadhaa kaunti ya Mombasa ikiwemo wizi wa kimabavu na biashara haramu.

Washukiwa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Changamwe wakitarajiwa kushtakiwa mahakamani wakati wowote.

Comments

comments