Tapeli Apora Maelfu Ya Pesa Kutoka Kwa Wakazi Wa Taita Taveta.

Tapeli Apora Maelfu Ya Pesa Kutoka Kwa Wakazi Wa Taita Taveta.

by -
0 441

Baadhi ya wenyeji katika kaunti ya Taita Taveta, wanadai kutapeliwa na mtu anayewaahidi kazi katika serikali ya Kaunti.

Mwanamume huyo alidaiwa kutapeli watu kwa kutumia jina la gavana wa Taita Taveta John Mrutu na maafisa wengine wa kaunti hiyo.

Jesmily Ngele mwenye umri wa miaka 21, alidai kumpa mwanamume huyo shilingi elfu 13 akisema pesa hizo ni za kuharakisha ajira kwa kuzigawanyia maafisa tofauti wa serikali hiyo, ili wapitishe uajiri wake.

Lakini gavana Mruttu, aliwataka wakaazi kuwa waangalifu zaidi na kutoa ripoti kwa vyombo husika ili hatua mwafaka zichukuliwe.

Comments

comments