Serikali Yatoa Shilingi Milioni 500 Kukabili Kipindupindu.

Serikali Yatoa Shilingi Milioni 500 Kukabili Kipindupindu.

by -
0 460

Hazina ya kitaifa imetoa shilingi nusu bilioni za kukabili maradhi ya kipindupindu nchini,ambayo kufikia sasa yameuwa watu 65.

Katibu wa wizara ya afya Khadijah Kassachoon, amesema wizara hiyo imo mbioni kuhakikisha ugonjwa huo hausambai.

Kassachoon alisema pesa hizo zitatumika kununua vifa vya matibabu,kusambaza maji safi, kuhamasisha umma na pia kuwezesha serikali za kaunti kukabili kipindupindu.

Kaunti 11 ikiwemo Mombasa zimeathiriwa na maradhi ya kipindupindu.

Hayo yanajiri siku chache tangu wafungwa wawili wa gereza la Shimo La Tewa hapa Mombasa, kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Wengine 30 walitengwa ili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Comments

comments