Mwili Mwingine Wapatikana Ndani Ya Kisima Likoni.

Mwili Mwingine Wapatikana Ndani Ya Kisima Likoni.

by -
0 646

Mwili mwingine wa mwanamme wa umri wa makamo umepatikana ndani ya kisima karibu na msikiti Bilaal eneo la Majengo mapya wilayani likoni jijini Mombasa.

Maiti hiyo ambayo ilikuwa imeharibika, ilipatikana na wakaazi kufuatia harufu iliyokuwa ukitoka ndani ya kisima hicho.

Maiti hiyo haikuweza kutambuliwa na inakisiwa ni mtu aliuliwa kwingine kisha kutupwa ndani ya kisima hicho.

Mkuu wa polisi wilayani Likoni Willy Simba alisema wataalam wanashughulikia simu iliyopatikana ndani ya kisima hicho, inayoaminikika kuwa ya marehemu ili kubaini maiti hiyo.

Comments

comments