MSF Yagadhabishwa Na Wapiganaji Sudan Kusini

MSF Yagadhabishwa Na Wapiganaji Sudan Kusini

by -
0 529

Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF linataka wapiganaji nchini Sudan Kusini kuheshimu haki za raia.

Mkuu wa shirika hilo nchini Sudan Kusini Paul Critchley amesema vita hivyo vimesababisha hospitali nyingi kufungwa na idadi kubwa ya wananchi kukosa matibabu.

Critchley ameeleza kughadhabishwa na wapiganaji hao, kwa kuwa baadhi yao wanavamia taasisi za matibabu.

Amesema wananchi wengi wamekuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani mbali na kukosa maji safi na chakula.

Taarifa ya shirika hilo la MSF imetolewa na mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano Wairimu Gitau katika mazungumzo na waandishi wa habari jijini Nairobi.

Comments

comments