Kesi Ya “Warembo wa Al-shabaab” Kuendelea Kortini Mombasa.

Kesi Ya “Warembo wa Al-shabaab” Kuendelea Kortini Mombasa.

by -
0 865

Kesi ya wasichana wanne wanaoshukiwa kuwa washirika wa kundi la Al Shabaab, imeahirishwa katika mahakama ya hapa Mombasa.

Wasichana hao ambao ni wanafunzi Ummul-kher Abdullah raia wa Tanzania pamoja na Wakenya Khadija Abdulkadir na Mariam Aboud, walikamatwa eneo la Elwak huko Wajir kwa madai ya kutaka kuvuka mpaka kuingia nchini Somalia ili kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabab.

Kundi hilo la Al-shabaab limehusishwa na mauaji ya watu wengi humu nchini kutokana na mashambulizi ya kigaidi,tangu jeshi la Kenya KDF kuingia Somalia mwaka 2011.

Mshukiwa wa nne Khalima Adan Ali alikamatwa mwezi jana eneo la Kyuvi kaunti ya Machakos, ambako alikuwa mfanya-biashara

Hakimu Richard Odenye ambaye anatarajiwa kutoa uamuzi wa kuwaachiliwa wasichana hao kwa dhamana, amesema ombi lao litasikiswa Ijumaa hii

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES