Mwili Wa Mwanamke Wapatikana Majini-Kibarani.

Mwili Wa Mwanamke Wapatikana Majini-Kibarani.

by -
0 541

Mwili wa mwanamke mmoja mwenye umri wa makamo umepatikana ukielea majini eneo la kibarani hapa Mombasa.

Kulingana na walioshuhudia, mwili huo uligunduliwa na wavuvi waliokuwa wakiendesha shughuli zao za uvuvi siku ya alhamisi alfajiri.

Mwili huo ulisemekana ulikuwa na kamba shingoni na kwamba huenda mwanamke huyo alibakwa kabla ya kuuliwa na mwili wake kutupwa majini.

Eneo hilo la kibarani, limetajwa kuwa hatari kwa usalama haswa giza linapoingia,kutokana na miili ya watu ambayo hupatikana hapo mara kwa mara.

Majuma kadhaa yaliyopita, mwili wa mwanamume mmoja ulipatikana ukielekea majini eneo hilo na inakisiwa pia huenda aliuawa.

Taarifa zaidi imeandikwa na George Otieno

Comments

comments