#MshukiwaWaUgaidi “Ashakufa” Mahakama Yaambiwa

#MshukiwaWaUgaidi “Ashakufa” Mahakama Yaambiwa

by -
0 344

Utata umeibuka kufuatia taarifa za kifo cha mshukiwa wa ugaidi, aliyekuwa miongoni watu waliokamatwa mapema mwaka 2014 katika mtaa wa Majengo kaunti ya Mombasa.

Utata huo umeripotiwa mahakamani Mombasa kuhudiana na kesi ya washukiwa 29, walionaswa mwaka jana katika msikiti Masjid Mussa.

Familia ya mshukiwa huyo kwa jina Ibrahim Mohamed Abdi inasema kuwa alifariki na tayari amezikwa.

Wakili wa washukiwa Chacha Mwita amesema cheti cha kudhibitisha kifo cha Ibrahim kiliwasilishwa mahakamani Mombasa.

Lakini yasemekana kuwa Chifu wa mtaa wa Timbwani anakotoka mshukiwa huyo, hakuonyeshwa mwili wa marehemu licha ya kuarifiwa kuwa alifariki.

Utata kuhusu kifo cha mshukiwa huyo wa ugaidi ulisababisha mahakama ya Mombasa kuipa idara ya upelelezi muda zaidi, wa kuchunguza iwapo mshukiwa huyo aliaga dunia.

Hii ni baada ya Simon Simiyu -afisa wa upelelezi katika kesi hiyo, kuomba mahakama muda wa siku 21.

Ibrahim Moh’d Abdi alikuwa miongoni mwa vijana zaidi ya 100 waliokamatwa na polisi Februari mwaka 2014, kwa madai ya kupokea mafunzo ya kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Comments

comments