Wafungwa Wafariki Gereza La Shimo La Tewa Kutokana na Kipindupindu.

Wafungwa Wafariki Gereza La Shimo La Tewa Kutokana na Kipindupindu.

by -
0 1409

Wafungwa wawili wameripotiwa kufariki kutoka na maradhi ya kipindupindu katika gereza la Shimo la tewa hapa Mombasa.

Mfungwa mmoja alifariki jana usiku na mwengine ameaga dunia mapema jumatano.

Watatu walilazwa katika hospitali ya Makadara kwa matibabu.

Tayari maafisa wa kaunti ya Mombasa wamepeana dawa kwa waathiriwa.

Sehemu zingine za pwani zilizoipotiwa kuwepo hofu ya maradhi hayo ni Voi,ambapo uuzaji vyakula hasa vya kupika umepigwa marufuku na serikali ya kaunti hiyo.

Watu kadhaa nchini semeu za Nakuru na Nyeri na hata hapa Mombasa katika mtaa wa Likoni, watu kadhaa walipotea maisha yao kutokana na kipindupindu.

Comments

comments