Kaunti Ya Mombasa Kununua Magari 25 Ya Askari Wake.

Kaunti Ya Mombasa Kununua Magari 25 Ya Askari Wake.

by -
0 380

Serikali ya kaunti ya Mombasa inasema itanunua magari 25 zaidi kwa askari wa kaunti.

Khamisi Mwaguya ambaye ni Katibu katika kaunti ya Mombasa, anasema magari hayo yatakuwa na vifaa vya kisasa vya mawasiliano ikiwepo kamera za kiusalama zinazoweza kunasa picha kutoka umbali wa mita 500.

Mwaguya amesema magari hayo yatasambazwa katika maeneo ya Mwakirunge, Shika Adaba, Miritini na maeneo mengine yanayoshuhudia utovu wa usalama.

Magari mengine 12 ya maaskari wa kaunti yalitolewa julai mwaka jana, japo haijabainika gharama yake.

Comments

comments