Gavana Joho Ashtumu Ubomoaji Wa Majengo Na Vibanda Changamwe.

Gavana Joho Ashtumu Ubomoaji Wa Majengo Na Vibanda Changamwe.

by -
0 490

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imeshtumu ubomoaji wa majengo na vibanda eneo la Magongo huko Changamwe unaodaiwa kutekelezwa na mamlaka ya kitaifa ya ujenzi wa barabara.

Gavana Hassan joho aliwaagiza walioathirika na ubomoaji huo kurudi kazini na kuendelea na biashara zao kama kawaida.

Ubomoaji huo unadaiwa kuendeshwa ili kupisha upanuzi wa barabara.

Gavana Joho alisema halmashauri hiyo ilibomoa majengo ya wafanyibiashara hao bila kuhusisha serikali ya kaunti.

Aliwaagiza wafanyabiashara hao wa JuaKali kurudi katika mahala pao pa kufanya biashara hadi pale hamlmashauri hiyo itawapa mahala pengine mbadala pa kufanyia biashara.

Wafanyi biashara hao wa Jua kali nao walisema wanakadiria hasara kubwa kutokana na ubomoaji huo.

Comments

comments