Makumi Ya Vijana Wakamatwa Kuhusiana Na Ulanguzi Wa Mihadarati Mombasa.

Makumi Ya Vijana Wakamatwa Kuhusiana Na Ulanguzi Wa Mihadarati Mombasa.

by -
0 578

Maafisa wa polisi wakishirikiana na askari wa kaunti ya Mombasa, wamekamata zaidi ya vijana 60 wanaohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya na wizi wa kimabavu.

Vijana hao wamekamatwa kufuatia oparesheni iliyoendeshwa wilayani Kisauni jijini Mombasa.

Oparesheni hiyo ilifanyika usiku wa kuamkia jumanne maeneo ya Kisauni-Magodoroni, Bamburi na Bombolulu.

Vitambulisho vya kitaifa, kadi za ATM na vifaa vingine vilipatikana kutoka kwa washukiwa.

Mtaa wa Magodoroni ni eneo lililotajwa kuwa hatari kwa usalama kwani ni ngome kuu ya watumiaji wa dawa za kulevya maarufu “mateja”, ambapo vijana wengi wamekuwa wakiwapora abiria wanaotumia barabara ya Bamburi Kisauni.

Mkuu wa kitengo cha ukaguzi kaunti ya Mombasa Charles Changawa aliwataka wote waliopoteza vitambulisho vyao kufika ofisi za askari wa kaunti eneo la Tudor.

Comments

comments