Mahakama Kutembelea Boma La Mfugaji Nyoka Huko Kwale.

Mahakama Kutembelea Boma La Mfugaji Nyoka Huko Kwale.

by -
0 509

Mahakimu katika mahakama ya Kwale wanatarajiwa kuzuru katika kijiji cha Mwamanga nyumbani kwa mtu aliyekamatwa kwa kuwafuga nyoka na wanyamapori bila kibali.

Hii ni baada ya mshukiwa kushtakiwa katika mahakama hiyo jana, ambapo alikiri kuwafuga nyoka wanne aina ya chatu na kobe 24 .

Mahakimu wanaoskiza kesi hiyo watazuru nyumbani kwa mshukiwa ili kuendeleza uchunguzi wao.
Mshukiwa huyo ana umri miaka 50.

OCPD wa Msambweni Joseph Omijah, alitaja jina la mshukiwa huyo kama Raphael Galozi na alifikishwa kortini Kwale jumatatu.

Comments

comments