Jumba La Orofa Labomolewa Nyali.

Jumba La Orofa Labomolewa Nyali.

by -
0 334

Jumba la ghorofa nne katika eneo la Gachanga-Nyali hapa Mombasa ambalo sehemu yake ilianguka jana jumapili, hatimae limebomolewa kabisa.

Lakini mmiliki wa jumba hilo alikataa kwamba jumba hilo liliporomoka na badala yake alidai kuwa huenda ilikuwa ni njama ya watu fulani kumhujumu kwa kubomoa jumba lake.

Kauli hiyo hata hivyo ilipingwa vikali na katibu wa ardhi na mipango kaunti ya Mombasa Francis Thoya, ambaye aliongoza shughuli za kubomoa jumba hilo akisema kanuni za ujenzi hazikuzingatiwa.

Jumba hilo la mamilioni ya pesa, liliporomoka lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Comments

comments