Mtu Akamatwa Msambweni Kwa Kuwafuga Nyoka.

Mtu Akamatwa Msambweni Kwa Kuwafuga Nyoka.

by -
0 551

Polisi eneo la Msambweni kaunti ya Kwale, wanamzuilia mwanmme mmoja aliyepatikana akifuga Nyoka na Kobe bila kibali.

Mwanamme huyo alikamatwa katika kijiji cha Mwamanga akiwafuga nyoka wanne na kobe 24.

Mkuu wa polisi Msambweni Joseph Omijah, alisema mshukiwa alikuwa akiwafuga nyoka aina ya chatu bila kibali kutoka shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS.

Mshukiwa anatarajiwa kushtakiwa mahakamani jumatatu.

Comments

comments