Mtu Akamatwa Kwa Madai Ya Kusajili Vijana Kujiunga Na Al-shabaab.

Mtu Akamatwa Kwa Madai Ya Kusajili Vijana Kujiunga Na Al-shabaab.

by -
0 450

Mshukiwa aliyekamatwa huko Likoni kwa tuhuma za kusajili vijana na kuwasafirisha nchini Somalia kujiunga na kundi la Al Shabaab, atashtakiwa mahakamani jumatatu.

Abdallah Salim alikamatwa juzi na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Makupa hapa Mombasa.

Mshukiwa alikamatwa nyumbani kwake mtaa wa manyatta huko likoni na kusafirishwa chini ya ulinzi mkali, lakini familia yake imekana kuwa mshukiwa anahusika na visa hivyo.

Kundi la kigaidi la Al-shabaab limekuwa kero kubwa humu nchini kufuatia visa vya kigaidi na mauaji ya watu wengi.

Comments

comments