Watu Wawili Washtakiwa Kortini Kwa Kumbaka Msichana Mlemavu.

Watu Wawili Washtakiwa Kortini Kwa Kumbaka Msichana Mlemavu.

by -
0 422

Wanaume wawili wameshtakiwa mahakamani Mombasa kwa madai ya kumbaka msichana mlemavu mwenye umri wa miaka 16.

Sammy Athuman na Bakari Kadenge, walidaiwa kumbaka msichana huyo asiye na uwezo wa kusikia, siku ya Jumatatu ya Mei tarehe 4, eneo la Likoni hapa Mombasa.

Vijana hao walidaiwa kumbaka msichana huyo walipomhadaa kwamba watampa peremende na nyama, kulingana na mlalamishi aliyeambia mahakama kwa lugha ya ishara.

Mahakaam ilikubali ombi la Mwendesha mashtaka kwamba washukiwa wapelekwe katika kituo cha polisi cha Inuka huko Likoni, ili kufanyiwa uchunguzi zaidi kuhusu ubakaji.

Kesi hiyo itatajwa mahakanai Ijumaa ijayo, ambapo mashahidi watano wanatarajiwa kuitwa kutoa ushahidi wao.

Comments

comments