Washukiwa Wa Ujambazi Wanaswa Mombasa.

Washukiwa Wa Ujambazi Wanaswa Mombasa.

by -
0 398

Washukiwa wanne wa ujambazi wamekamatwa katika mtaa wa Old Town hapa Mombasa, kwenye oparesheni Iliyoendeshwa na maafisa wa polisi wa GSU wakisaidiwa na mbwa wa kunusa.

Washukiwa hao ambao walitambuliwa kwa majina kama Rasta shehe, Yussuf Hassan Yusuf na Abdurma Marko, walikamatwa na wanazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Visu 5 na kofia ya jeshi vilipatikana kutoka kwa nyumba ya mshukiwa mmoja.

Polisi walisema mshukiwa mmoja ambaye alitoroka, huenda alikuwa na bunduki na sasa wameanzisha oparesheni nyingine ya kumsaka.

Lakini familia ya mshukiwa mmoja, ilikana kuwa jamaa yao amekuwa akihusika na uhalifu japo walikiri kuwa aliwahi kuhukumiwa jela miaka mingi iliyopita.

Comments

comments