Mshukiwa Wa Wizi Achomwa Likoni.

Mshukiwa Wa Wizi Achomwa Likoni.

by -
0 411

Wananchi waliokuwa na hamaki wamemchoma mshukiwa mmoja wa wizi kiasi cha kutotambulika katika mtaa wa Ushindi Likoni hapa Mombasa.

Yasemekana mshukiwa huyo kwa jina Amos Mwendwa Mutie mwenye umri wa miaka 23, alinuia kutekeleza wizi katika duka moja la M-Pesa akitumia bunduki bandia.

Lakini wananchi walimkamata na kumchoma moto, pindi walipogundua kwamba bunduki aliyokuwa nayo ilikua bandia.

Afisa mkuu wa upelelezi eneo la Likoni David Siele, alisema wanasaka genge la majambazi linaloaminika lilipanga njama hiyo lakini washukiwa wengine wakatoroka mtego wao ulipotibuka.

Comments

comments