Mabaki Ya Miili Ya Watu Yafukuliwa Kupisha Ujenzi wa Reli Kwale.

Mabaki Ya Miili Ya Watu Yafukuliwa Kupisha Ujenzi wa Reli Kwale.

by -
0 415

Mabaki ya miili 14 ya watu imefukuliwa eneo la Mgalani-Taru kaunti ya Kwale, ili kutoa nafasi ya ujenzi wa reli ya kisasa.

Wenyeji wa sehemu hiyo walipewa notisi ya siku 12 kufukua miili hiyo kwa malipo na kuizika kwengineko la sivyo ujenzi wa reli hiyo uanze bila ya miili hiyo kufukuliwa.

Wakaazi hata hivyo walilalama kuhusu kiwango cha fedha waliyolipwa kusimamia shughuli ya kufukua miili na kuizika kwingineko, wakisema ni kidogo.

Miili hiyo ilizikwa tena katika sehemu tofauti.

Miezi miwili iliyopita wanakajiji wa Kafuduni A na Kafuduni B kaunti hiyo ya Kwale, walilipwa shilingi elfu hamsini kwa kila kaburi, kusimamia maziko upya,ili kupisha mradi wa reli hiyo ya kisasa itakayofika hadi nchi za Sudan Kusini na Rwanda.

Comments

comments