Gavana Kingi Aondolewa Lamawa Kuhusu Jumba la Shilingi Milioni 140.

Gavana Kingi Aondolewa Lamawa Kuhusu Jumba la Shilingi Milioni 140.

by -
0 596

Ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma Keriako Tobiko imemwondolea lawama gavana wa Kilifi Amerson Kingi kuhusu ununuzi wa kasri lake lililogharimu shilingi milioni 140.

Kupitia barua kwa vyombo vya habari, Tobiko amesema ripoti ya uchunguzi wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC, imeonyesha kwamba Kingi alizingatia sheria zote katika kununua nyumba hiyo na kwamba hakukuwepo ubadhirifu wa pesa ua utumizi mbaya wa fedha.

Tobiko amesema uchunguzi wa tume ya kukabili ufisadi EACC, haukumpata Kingi na kosa lolote na imependekeza faili kuhusu kesi hiyo ifungwe.

Hata hivyo mwendesha mashtaka wa umma, amependekeza wanachama wa kamati ya zabuni ya kaunti hiyo pamoja na katibu wa kaunti na mkuu wa hazina ya kaunti hiyo ya Kilifi, kuchukiliwa hatua za kinidhamu kwa kutowajibika kikamilifu kazini.

Comments

comments