Serikali Yafuatilia Habari Za Meli Inayodhaniwa Kubeba Silaha.

Serikali Yafuatilia Habari Za Meli Inayodhaniwa Kubeba Silaha.

by -
0 391

Meli inayoaminika kusheheni zana za kivita imekuwa ikifuatiliwa baharini na inatarajiwa bandarini Mombasa wakati wowote kuanzia sasa.

Meli hiyo ambayo hadi sasa haijabainika ilinuiwa kusafirisha silaha hizo wapi, inaaminika kugunduliwa na jeshi la wana maji wa Kenya.

Taarifa za kijasusi zinasema haijabainika meli hiyo imetokea nchi gani.

Kuna taarifa zisizoaminika kuwa huenda zana hizo za kivita, zilipaswa kusafirishwa katika nchi ambazo zinashuhudia mgogoro wa kivita.

Comments

comments