Wakazi Wa Wundanyi Waandamana Kulalamikia Barabara Mbovu.

Wakazi Wa Wundanyi Waandamana Kulalamikia Barabara Mbovu.

by -
0 460

Wakaazi wa eneo bunge la Wundanyi kaunti ya Taita Taveta, wamefanya maandamano kushinikiza serikali ikarabati barabara kuu ya kutoka Wundanyi kuelekea Mwatate.

Wakingozwa na wawakilishi wa wodi tofauti katika kaunti hio, wakaazi hao wamelalamikia hali mbovu ya barabara hiyo, jambo wanalosema limeathiri pakubwa usafiri.

Lakini serikali ya kaunti hiyo ilisema italazimika kutenga fedha kukarabati barabara hiyo japo jukumu ni la serikali kuu, ili kurahisisha usafiri, huku ikisubiri serikali ya kitaifa kutekeleza wajibu wake kulingana na sheria.

Haya yanajiri wiki moja baada ya wanaharakati katika kaunti hio kujitokeza wakitaka maelezo kamili kuhusiana na ukarabati wa bara bara hiyo kutoka kwa serikali ya kitaifa.

Comments

comments