Mvuvi Apatikana Kilifi Amefariki Akidaiwa Kuuawa.

Mvuvi Apatikana Kilifi Amefariki Akidaiwa Kuuawa.

by -
0 546

Maafisa wa polisi huko Kilifi wanachunguza mauaji ya mtu mmoja mvuvi, anayedaiwa kuuawa na mwili wake kutupwa baharini.

Mwili wa mwanamume huyo ambaye jina lake ni George Chengo Kibiribiri, ulipatikana mapema jumatano ukiwa na alama za kuashiria kuwa alidungwa kwa kisu.

Afisa mkuu wa polisi eneo la kilifi Justine Nyaga, aliambia Baraka FM kwamba marehemu ni mtu mwenye umri wa miaka 60.

Wavuvi wenzake walisema marehemu, alifungwa mikono kwa kutumia kamba, huku mwili wake ukielea baharini.

Mwili wa mvuvi huyo ulipelekwa katika chumba cha maiti cha hospitali kuu ya Kilifi.

Comments

comments