Mume Wa Umri Wa Miaka 40 Auawa Kinyama Huko Kilifi.

Mume Wa Umri Wa Miaka 40 Auawa Kinyama Huko Kilifi.

by -
0 474

Mwanamume mmoja wa miaka umri wa 40 ameuawa usiku wa jumanne na watu wasiotambulika eneo la Tezo kaunti ya Kilifi.

Marehemu aliyetambulika kwa jina Tunje Juba Starnley, alivamiwa na genge la watu watatu waliokuwa wamejihami kwa upanga na shoka.

Marehemu aliuawa kwa kukatwa upanga shingoni akiwa nyumbani kwake.

Mwili wake unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Kilifi.

Hayo yakitokea mtu mmoja amefariki dunia huku wengine 9 wakijeruhiwa, baada ya Timbo kuporomoka katika kijiji cha Vitengeni kaunti ya kilifi.

Taarifa zinasema kuwa watu hao walikuwa wakichimba mchanga kabla ya kufunikwa na mchanga huo mwepesi kutokana na mvua kubwa inayonyesha.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Bamba, waliondoa maiti ya mwathiriwa na kuwataka wote wanaoendeleza uchimbaji kusitisha shughuli hiyo hadi pale mvua itakapopungua.

Comments

comments