Kijana Atupwa Jela Kwasababu Ya Wizi NdogoNdogo.

Kijana Atupwa Jela Kwasababu Ya Wizi NdogoNdogo.

by -
0 342

Mahakama ya Mombasa imemhukumu kifungo cha miaka 6 gerezani, kijana mmoja alivunja nyumba na kuiba.

Hakimu Richard Odenyo alitoa hukumu hiyo baada ya mshukiwa huyo kwa jina Menza Nyamai kukiri kuwa alitekeleza uhalifu huo katika mtaa wa Likoni Mombasa.

Nyamai mwenye umri wa miaka 22 alidaiwa kuvunja nyumba na kumwibia Abdul Karim Konde mali ya shilingi elfu 13,mwezi februari katika eneo la Makao Mema wilaya ya likoni.

Kijana huyo alipatikana na hatia ya kuvunja nyumba hiyo na kuiba pesa,nguo za thamani ya shilingi elfu sita,viatu vya shilingi elfu moja mia mbili na cheti cha kuendesha gari.

Mahakaa hiyo ilimpaa siku 14 za kukata rufaa.

Comments

comments