Seneta Mwazo Apendekeza Nyongeza Ya Mgao Wa Fedha

Seneta Mwazo Apendekeza Nyongeza Ya Mgao Wa Fedha

by -
0 618

Pendekezo limetolewa kuongezwa kwa mgao wa fedha katika serikali za kaunti hadi asilimia 45,ili kudhibiti ugatuzi kikamilifu.

Seneta wa kaunti ya Taita Taveta Dan Mwazo alisema iwapo pesa hizo zitaongezwa zitasaidia kuleta maendeleo mashinani.

Mwazo pia alisema serikali za kaunti zinaweza kuongezewa majukumu zaidi endapo fedha hiyo itaongezwa.

Alidokeza kuwa katiba ya nchi ni lazima ifanyiwe mabadiliko katika baadhi ya vipegee hasa vinavyoleta utata miongoni mwa wananchi.

Comments

comments