Mwanamume Ashtakiwa Kwa Madai Ya Kumpiga Polisi

Mwanamume Ashtakiwa Kwa Madai Ya Kumpiga Polisi

by -
0 355

Mtu mmoja ameshtakiwa mahakamani Mombasa kwa madai ya kumpiga na kumjeruhi afisa wa polisi.

Jackson Munuri Kimau pamoja na wenzake ambao hawajashtakiwa, wanadaiwa kumjeruhi afisa wa polisi kwa jina Said Jarson eneo la Chaani huko Changamwe.

Mahakama iliambiwa kuwa bunduki na risasi 30 zilitoweka wakati huo, na kuwa afisa huyo wa polisi yuko katika hali mahututi hospitali akiendelea kuuguzwa.

Mwanamume huyo amekana mashtaka mbele ya hakimu Richard Odenyo, na kesi hiyo itatajwa Julai tarehe 7.

Comments

comments