#WatotoPacha Waliozaliwa na Baba Tofauti

#WatotoPacha Waliozaliwa na Baba Tofauti

by -
0 811

Mwanamke mmoja katika jimbo la New Jersey nchini Marekani ameshtushwa na habari kuwa watoto wake pacha wenye umri wa miaka miwili unusu, wamezaliwa na baba tofauti.

Uchunguzi wa kitaalamu kutoka chembe-chembe za DNA umebaini kuwa mwanamke huyo alipata uja uzito wakati mmoja, baada ya kuonanan na waname wawili tofauti.

Kipitia uchuguizi huo wa DNA wataalamu wanasema watoto hao pacha, kila mmoja alipatikana kupitia yao lenye mbegu ya baba tofauti.

Mwanamme huyo aliyetajwa kwa jina la “T.M” alipata majibu hayo ya kushangaza kupitia stakabadhi za mahakama siku ya Alhamisi, akitaka baba ya watoto wake ashinikizwe kuwalea.

“T.M.” alikuwa ameeleza kimasomaso kuwa wiki anayoamini kutunga mimba, pia alionana kimwili na mtu aliyekuwa mpenzi wake wa zamani.

Sasa uchunguzi wa DNA umedhihirisha kuwa mumewe ni baba ya pacha mmoja tu, na pacha wa pili ni mtoto wa mpenziwe.
Picha tuliyoweka hapo juu kuambatana na taarifa hii sio picha halisi ya watoto hao wasichana.

Umri wao sasa unaelekea miaka mitatu.

Comments

comments