Mafuriko Yatatiza Wakaazi Mombasa.

Mafuriko Yatatiza Wakaazi Mombasa.

by -
0 629

Wakaazi wengi wa mitaa ya mabanda hapa Mombasa sasa wanakosoa serikali ya kaunti kutokana na athari za mvua kubwa zinazowakumba.

Waathiriwa hao walisema wamepoteza makaazi yao na hata kukadiria hasara katika biashara zao kutokana na mafuriko.

Walisema wanahofia huenda nyumba zaidi zikasombwa maji, iwapo serikali ya kaunti ya Mombasa, haitainukia na mpango mwafaka wa kudhibiti mafuriko.

Lakini hayo yanajiri huku nao mawaziri katika kauntihiyo, wakirushiana lawama kuhusu mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa hapa Mombasa.

Waziri wa ardhi na mipango Francis Thoya na mwenzake wa maji na mazingira Fatma Awale, wote wanadai swala la mafuriko halipo chini ya wizara zao.

Hii ni licha ya mitaa ya Mwandoni -Kisauni, Bakarani na Utange na Mikindani kushuhudia mafuriko ambao yamesababisha hasara.

Aidha imebainika kuwa miundo msingi duni kama ukosefu wa mitaro ya maji, na ukosefu wa mipangilio ya ujenzi wa nyumba imechangia hali hii.

Comments

comments