Vijana 12 Rabai Na Kaloleni Wasajiliwa Kujiunga Na Kikosi Cha Askari Jela.

Vijana 12 Rabai Na Kaloleni Wasajiliwa Kujiunga Na Kikosi Cha Askari Jela.

by -
0 518

Jumla ya vijana 12 maeneo ya Kaloleni na Rabai, wamesajiliwa kujiunga na kikosi cha askari wa magereza katika zoezi lililokamilika jumatano.

Eneo la Kaloleni, vijana 6 walifaulu kuchukuliwa wakiwemo wasichana wawili na wavulana wanne na huko Rabai, idadi sawia ya hiyo ikachukuliwa.

Msimamizi wa zoezi hilo katika eneo la Kaloleni supretendant Josphene Mutuku, alisema mvua kali iliyonyesha siku nzima ilitatiza usajili huo japo watu wengi walijitokeza.

Mutuku alipongeza vijana wa sehemu hiyo kwa kutikia mwito na kujitokeza kwa zoezi hilo la usajili wa makurutu wa askari wa magereza.

Na huko Rabai, zoezi lilianza jioni na kukamilika usiku,kufuatia mvua kubwa iliyonyesha sehemu hiyo huku vijana wakiamua kupiga kambi uwanja wa mkapuni siku nzima, hadi shughuli ikaanza saa kumi na mbili jioni na kukamilika saa mbili usiku.

Lakini maeneo mengi hapa Mombasa, kulikuwa na hali ya sitofahamu,duru zikisema huenda zoezi halikufanyika.

Katika eneo la Mvita, shughuli wala maafisa wa kusimamia zoezi hilo hawakuonekana.

Comments

comments