Mawaziri Wa Mombasa Warushiana Lawama Juu Ya Mafuriko.

Mawaziri Wa Mombasa Warushiana Lawama Juu Ya Mafuriko.

by -
0 596

Mawaziri katika kaunti ya Mombasa sasa wanarushiana lawama kuhusu mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa hapa Mombasa.

Waziri wa ardhi na mipango Francis Thoya na mwenzake wa maji na mazingira Fatma Awale, wote walidai swala la mafuriko halipo chini ya wizara zao.

Hii ni licha ya mitaa ya Mwandoni -Kisauni, Bakarani, Utange na Mikindani kushuhudia mafuriko ambayo yamesababisha hasara na barabara kuziba.

Waziri Thoya, aliondolea wizara yake lawama akisema kamwe haihusiki na masuala ya mitaro wala mazingira, huku naye waziri Awale, akiondolea wizara yake lawama na badala yake akitupia lawama, lililokuwa baraza la manispaa na wakazi.

Katika mtaa wa Bakarani, maji yanayotokana na mvua, yalijaa hadi majumba ya watu na kuharibu mali ya maelfu ya pesa,huku familia kadhaa zikilazimika kulala nje.

Imebainika kuwa miundo msingi duni kama ukosefu wa mitaro ya maji, na ukosefu wa mipangilio ya ujenzi wa nyumba imechangia hali hii.

Hayo yanjiri huku utabiri wa hali ya anga ukieleza kuwa mvua hiyo inayonyesha sehemu nyingi nchini itaendelea kwa majuma kadhaa.

Comments

comments