Uhamisho Wa Mahakimu Watatiza Shughuli Za Mahakama Ya Mombasa.

Uhamisho Wa Mahakimu Watatiza Shughuli Za Mahakama Ya Mombasa.

by -
0 673

Mahakama za hapa Mombasa zinakumbwa na uhaba wa mahakimu na makarani, baada ya waliokuwa wakihudumu katika mahakama hiyo kupewa uhamisho.

Hapo jana jumanne, kesi nyingi hazikuweza kusikilizwa kortini Mombasa kutokana na uhaba wa mahakimu hao na pia makarani.

Wakili wa kesi ya mshukiwa wa ulanguzi wa pembe za ndovu Faisal Mohamed, aliilaumu idara ya mahakama humu nchini, baada ya kuhamisha mahakimu hao kwa wakati mmoja.

Wakili huyo Jared Magolo alisema hatua hiyo huenda ikahujumu usikilizaji wa kesi za awali na hata zingine kuanzishwa upya.

Magolo alidokeza kuwa mahakimu na makarani wamepewa uhamisho katika mahakama nyingi nchini.

Mahakimu wapya wanatarajiwa kuripoti wiki hii hapa Mombasa.

Hayo yakijiri hakimu wa Mombasa Stephen Riech, amepandishwa cheo na kuwa jaji.

Uteuzi wake ulifanywa na rais Uhuru Kenyatta, kutokana na pendekezo la tume ya huduma za mahakama nchini JSC.

Comments

comments