Onyo Latolewa Kwa Walimu Wanaochochea Wanafunzi Kugoma Kilifi.

Onyo Latolewa Kwa Walimu Wanaochochea Wanafunzi Kugoma Kilifi.

by -
0 311

Idara ya elimu kaunti ya Kilifi inatoa onyo kwa walimu wanaochochea wanafunzi kushiriki migomo.

Mkurugenzi wa elimu kaunti hiyo- Dickson Ole Keis, alisema uchunguzi uliofanywa na idara ya elimu kaunti hiyo, umebaini kuwa walimu wanachangia migomo hiyo.

Ole Keis alisema walimu hao huchochea migomo kwa kuhofia matokeo mabaya ya wanafunzi kutokana na ulegevu wao kazini.

Alidokeza miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa dhidi ya walimu watakaopatikana na hatia ni kusimamishwa kazi au kupewa uhamisho.

Comments

comments