Mamia Ya Abiria Wakwama Taru-Maungu Kutokana Na Msongamano.

Mamia Ya Abiria Wakwama Taru-Maungu Kutokana Na Msongamano.

by -
0 407

Mamia ya abiria wamekwama maeneo ya Maungu, Taru na Mazeras kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi kutokana na msongamano mkubwa wa magari.

Mabasi ya usafiri kutoka Nairobi na sehemu zingine za nchi zimeripotiwa kukwama maeneo hayo, kwa muda wa saa 6,huku wasafiri wakilazimika kukesha ndani ya magari yao kutokana na msongamano huo mkubwa.

Sehemu kadhaa za barabara hiyo pia zimeripotiwa kufurika maji kutokana na mvua kubwa inayonyesha pwani.

Taswira hiyo ya msongamano mkubwa wa magari hushuhudiwa kila siku kuanzia mzunguko wa Changamwe kuelekea Jomvu-Mazeras hadi Mariakani kwenye barabara hiyo kuu.

Wasafiri wanaotumia barabara hiyo mara kwa mara wamekuwa wakililia serikali kuinuka na mbinu za kumaliza au kupunguza msongamano mkubwa wa magari wakisema wanapoteza muda mwingi barabarani.

Lakini mradi wa ujenzi wa reli mpya ya kisasa inayoendelea kwa sasa, inatarajiwa kuleta afueni kwa maelfu ya wasafiri wa barabara hiyo kuu ya Mombasa-Nairobi.

Comments

comments