Wanahabari Wa Baraka FM Wang’ara Tena Katika Tuzo.

Wanahabari Wa Baraka FM Wang’ara Tena Katika Tuzo.

by -
0 531

Kwa mara nyingine wanahabari wa Baraka FM wameshinda jumla ya tuzo 11 za baraza la vyombo vya habari nchini –MCK, mwaka huu wa 2015.

Wanahabari wetu wameshinda katika vitengo walivyoshiriki vya kuandika makala katika tuzo hizo ambazo hutolewa na baraza la vyombo vya habari kila mwaka.

Walioshinda tuzo ni pamoja na Josphat Kioko,Joseph Jira,Janet Kilalo na George Otieno.

Nao Diana Wanyonyi,Oscar Nyoha na Albert Mwangeka, walipata tuzo kwa kuibuka wa pili katika vitengo tofauti walivyoshiriki.

Kila mwaka Baraka FM imefaulu kuwa na kati ya wanahabari 3 na 5 katika tuzo mbali mbali za kitaifa na hata za kimataifa na hata kushinda nyingi, inapoadhimisha miaka 15 ya utangazaji bora.

Tunakukaribisha pia kuungana nasi katika kuadhimisha miaka 15 ya utangazaji bora.

Comments

comments