Polisi Mombasa Yatahadharisha Umma Kuhusu Washukiwa Hatari Wa Ugaidi.

Polisi Mombasa Yatahadharisha Umma Kuhusu Washukiwa Hatari Wa Ugaidi.

by -
0 386

Polisi hapa Mombasa wametaja washukiwa wanne wa ugaidi ambao picha zao zilitolewa na serikali wiki jana kuwa hatari kwa usalama wa nchi.

Ahmed Said Omar, Hussein Said Omar, Abdulkadir Abubakar na Issa Abdallah Kauni wanasemekana kupata mafunzo ya hali ya juu kutumia zana za kivita na wanamiliki silaha hatari, na pia walipanga kutekeleza mashambulio siku ya sherehe za Leba Day tarehe 1.

Kamanda wa polisi hapa pwani Robert Kitur, alisema madhara yaliepukwa, baada ya picha za magaidi hao kutolewa hadharani.

Hatua hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya polisi hapa Mombasa,kuweka mabango ya picha za washukiwa wa ugaidi wanaosakwa.

Comments

comments