Kampuni Za Uchimbaji Madini Kuchunguzwa Kaunti Ya Kilifi.

Kampuni Za Uchimbaji Madini Kuchunguzwa Kaunti Ya Kilifi.

by -
0 431

Serikali ya kaunti ya Kilifi imeanzisha zoezi la kukagua upya stakabadhi za uchimbaji madini kaunti hiyo, ili kupunguza athari kwa wakaazi wake.

Waziri wa mazingira, misitu na mali asili kaunti hiyo Kiringi Mwachitu, alisema wamepokea malalamishi kutoka kwa wakaazi hasa wanaoishi maeneo ya Ganze na Jaribuni.

Naye mwanahakati wa mazingira Mwanza Mwangiri, alisema wawekezaji wengi wa uchimbaji madini, wamekuwa wakikiuka kanuni za uchimbaji madini.

Alisema serikali ya Kilifi inafaa kuzidisha kasi yake ya kukabili swala hilo.

Comments

comments