Mkuu Mpya Wa Jeshi La KDF Achukua Ofisi.

Mkuu Mpya Wa Jeshi La KDF Achukua Ofisi.

by -
0 496

Mkuu mpya wa jeshi la Kenya KDF jenerali Samson Mwathethe, amechukua rasmi hatamu za uongozi.

Hafla ya kukabidhiwa hatamu na mkuu wa jeshi anayeondoka Julius Karangi, ilifanyika katika makao makuu ya jeshi eneo la DOD jijini Nairobi.

Mwathethe kutoka jeshi la wanamaji la Mtongwe hapa Mombasa, aliteuliwa mkuu mpya wa jeshi na rais Uhuru Kenyatta.

Mwathethe alizaliwa Malindi na kusomea shule za upili za Shimo La Tewa na Sacred Heart ,kabla ya kuijunga na Kenya Navy mwaka 1978.

Mkuu huyo wa jeshi ni msomi na pia amehitimu na shahada za mafunzo ya ofisa wa jeshi nchini Uingereza.

Comments

comments