Chifu Wa Zamani Atekwa Nyara Na Watu Wasiojulikana Huko Lamu.

Chifu Wa Zamani Atekwa Nyara Na Watu Wasiojulikana Huko Lamu.

by -
0 368

Familia moja mjini Lamu inaiomba serikali kuisaidia kumtafuta jamaa yao aliyetoweka kwa njia ya kutatanisha.

Mtu huyo anajulikana kama Hussein Mahmud mwenye umri wa miaka 67 na ambaye aliwahi kuhudumu kama Chifu wa Kata ya Kotile huko Ijara, kaunti ya Garissa.

Ni kisa ambacho kimeiacha familia hiyo na wasiwasi mwingi wasijue ikiwa jamaa wao yupo mikononi mwa walinda usalama au magaidi.

Jamaa yake mmoja alinukuliwa akisema Hussein alikamatwa na watu wasiofahamika ambao walimuingiza kwa lazia ndani ya gari moja kabla ya kutoweka na juhudi za kumpata hazijafaulu.

Sasa jamaa hao wanaitaka serikali kuisadia kujua alipo Mzee Hussein waliyemtaja kuwa mkamilifu na mpenda amani.

Haya yanajiri wakati ambapo familia nyingine mjini Lamu, bado ikiendelea kuhangaika kumtafuta kijana wao, Imrana Said Makka, anayedaiwa kutoroshwa na watu wasiojulikana alipokuwa ziarani mjini Malindi yapata mwezi mmoja uliopita.

Comments

comments