Watoto Wanne Wafariki Timboni Kwale.

Watoto Wanne Wafariki Timboni Kwale.

by -
0 878

Watoto wanne kutoka kaunti ya Kwale wameripotiwa kufariki baada ya kufunikwa katika timbo la mchanga.

Yasemekana watoto hao walikuwa wakicheza eneo la Maganyakulo huko Kombani walipokumbana na mauti.

Mtoto mwengine mmoja aliyekuwa pamoja nao alinusurika katika mkasa huo.

Polisi wa utawala kutoka kituo cha Kombani walidhibitishwa kuwa watoto hao walifariki Ijumaa jioni baada ya timbo hilo kuporomoka.

Miili yao ilipelekwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali kuu ya Msambweni.

Comments

comments