Mbio Za Dunia Bahamas (Relays)

Mbio Za Dunia Bahamas (Relays)

by -
0 549

Mashindano ya raidha ya ubingwa wa dunia kupokezana vijiti, yaani World Relays yanafanyika Jumamosi hii na JUmapili nchini Bahamas, Mei 2-3.

Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayowakilishwa katika mashindano hayo, ikiwa na matumaini ya kushinda tena dhahabu katika mbio za mita 800 mara 4 kupokezana vijiti.

Katika makala ya kwanza mwaka jana wa 2014 Kenya ilishinda dhahabu katika shindano hilo, na kuvunja rekodi ya dunia.

Katika mbio fupi mita 100 mara 4 na mita 200 mara 4 Usain Bolt wa Jamaica atakuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji, japo timu yake inakabiliwa na upinzani kutoka kikosi cha Marekani.

Takriban wanariadha 800 kutoka mataifa 40 wanashiriki mashindano hayo ya siku mbili, ambayo yamevutia watazamaji zaidi ya elfu 30.

Waandishi wa habari wapatao mia moja wako Bahamas kushuhudia mashindano hayo ya IAAF World Relays.

Comments

comments