Mbinu Zabuniwa Kuzuia Mimba Za Mapema Kwa Wasichana Wa Shule.

Mbinu Zabuniwa Kuzuia Mimba Za Mapema Kwa Wasichana Wa Shule.

by -
0 589

Eneo la Ganze huko Kilifi, imeanzisha mbinu mpya ya kukabiliana na mimba za mapema na dhulma za kimapenzi dhidi ya mtoto wa kike katika sehemu hiyo.

Mpango huo unahusisha kutembelea shule zote za msingi Ganze na kuandaa mikutano ya ushauri kwa wanafunzi umuhimu wa kujilinda na kuchukuliwa masomo yao kwa uzito badala ya kushirikia anasa.

Johnson Jefwa Yaa mwanzilishi wa mpango huo, alisema kando na kuwapa wanafunzi ushauri, mpango huo umeelekezwa hadi kwa wazazi,jambo ambalo alisema linasaidia pakubwa kupunguza visa hivyo.

Mara Kwa mara wasichana wengi wa kike eneo la pwani wamelazimika kuacha masomo,baada ya kupachikwa mimba za mapema na hata wengine wakiozwa mapema na wazazi wao.

Comments

comments